Sudan yawatimua maafisa wa UN

Image caption Mshirikishi mkuu wa utoaji msaada Ali Al-Zatariv

Umoja wa mataifa unasema kuwa Sudan imewafukuza maafisa wake wawili wakuu kutoka nchini humo.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-moon, amelishutumu taifa hilo kwa kumfurusha mshirikishi mkuu wa utoaji msaada Ali Al-Zatari, na mkurugenzi mkuu wa mpango wa maendeleo wa Umoja wa mataifa Nchini humo Yvonne Helle.

Haijafahamika ni kwa nini wawili hao wamefurushwa.

Uhusiano kati ya Umoja wa mataifa na serikali ya Sudan umekuwa m'baya tangu walinda amani wa umoja wa Afrika kuchunguza ripoti ya ubakaji ulioendeshwa na wanajeshi wa taifa hilo katika eneo la Darfur mwezi uliopita.