Tibaijuka:Nitatetea kiti changu

Image caption Aliyekuwa waziri wa Ardhi na makao nchini Tanzania Anne Tibaijuka anasema kuwa atatetea kiti chake cha ubunge licha ya kashfa ya Escrow

Siku kadhaa tu baada ya rais Kikwete kumfuta kazi Anne Tibaijuka kama waziri wa ardhi,nyumba na makao ,kiongozi huyo amewaambia wakaazi wa bunge lake kwamba hawakumchagua kama waziri bali kama mwakilishi wao wa bunge, kulingana na gazeti la The citizen nchini Tanzania.

Tibaijuka alipigwa kalamu kutokana na maadili yake kufuatia kashfa ya akaunti ya tageta escrow ambapo alipokea sh.billioni 1.6.'' Mungu anayetoa ndiye aliyechukua jina la mungu libarikiwe alisema tibaijuka akimaanisha kuwa yule aliyempa kiti hicho cha uwaziri ndiye aliyekichukua.

Katika kile alichoelezea kama harakati za kukitetea kiti chake katika uchaguzi wa 2015,Tibaijuka aliwaonya wapinzani wake wa kisiasa kwamba yeye ndiyo chagua bora la wapiga kura.

Kulingana na The Citizen kiongozi huyo aliwashukuru wapiga kura wa eneo bunge lake kwa kumchagua kuwa mbunge,wadhfa aliodai kumfungulia milango ya kupewa uwaziri.

''Lazima muelewe kwamba ninyi mulinipigia kura mimi ili niwahudumie bungeni na sio kama waziri,kwa hivyo yaliotokea si ndwele tugange yajayo kwa kuwa tayari kashfa ya escrow imezikwa'',aliwaambia wakaazi wa Muleba.

Hatahivyo bi Tibaijuka amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na viongozi wa upinzani waliochaguliwa katika uchaguzi wa madiwani wa hivi karibuni.