Feri ya abiria 460 yashika moto Ugiriki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Feri yashika moto ikiwa na abiria 460

Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na karibu abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki kwenda Italia.

Abiria waliokuwa kwneye ferry hiyo walipiga simu kwa vituo vya runinga nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na upepo unatatiza shughuli za uokoaji.

Maafisa wa ulinzi wa pwani nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman Atlantic ilikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati walipotuma ujumbe .

Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari.