Boko haram wavamia kijiji na kuua 15

Haki miliki ya picha AFP

Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.

Shambulizi hilo lilitokea katika kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye silaha, wakilenga askari wa ulinzi wa jadi wa mji huo.

Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, liliwateka nyara wasichana wa shule zaidi ya mia mbili mwezi Aprili mwaka huu.

Zaidi ya watu elfu kumi wameuwawa Nchini Nigeria na Boko Haram mwaka huu pekee.