Aua watu 8 naye ajiua Canada

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mmoja wa ndugu aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiomboleza mauaji ya ndugu yake

Polisi Nchini Canada wanasema kuwa watu 8 wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu mmoja ambaye naye alijiuua katika kile kilichotajwa kama mfululizo wa unyanyasaji wa majumbani.

Siku ya jumatatu polisi walikuta mwili wa mwanamke mmoja katika mji wa Edmonton eneo magharibi mwa jimbo la Alberta.

Polisi pia waliikuta miili mingine ambayo ni ya wanawake watatu,wanaume wawili na watoto wawili wakati ilipokuwa ikishughulikia taarifa ya mtu huyo aliyejiua katika eneo jingine kwenye mji huo.

Muuaji huyo alijiua mwenyewe kwenye mgahawa mmoja katika eneo la kaskazini mwa Edmonton.

Polisi bado haijatoa majina wala uhusiano wa waathirika.