Rais wa Gambia arudi nyumbani

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Gambia Yahya Jammeh

Ripoti kutoka Gambia zinasema kuwa rais Yahya Jammeh amerudi nchini humo kutoka ziara ya ughaibuni kufuatia njama ya kutaka kumpindua.

Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.

Haijulikani ni wapi rais Jammeh alikokuwa huku ripoti zikidai kuwa alikuwa nchini Ufaransa na wengine wakisema alikuwa Dubai.

Mkuu wake wa itifaki ameiambia BBC kwamba kila kitu kiko shwari katika mji mkuu.