Mfalme Abdullah wa Saudia alazwa

Haki miliki ya picha 1
Image caption Mfalme Abdullah wa saudia alazwa hospitalini

Mfalme Abdullah wa Saud Arabia amelazwa hospitalini ili kufanyiwa ukaguzi.

Taarifa kutoka kwa makao ya mfalme huyo haikutoa maelezo yoyote kuhusu hali yake.

Soko la hisa la Saudia lilianguka baada ya habari hizo kutangazwa katikan runinga ya taifa.

Mfalme Abdullah aliye na umri wa miaka 90 ametawala ufalme wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu mwaka 2005.