Rais mpya wa Tunisia ameapishwa

Image caption Rais Beji Caid Essebsi ameapishwa kama rais mpya wa Tunisia baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Tunisia

Rais mpya wa Tunisia Beji Caid Essebsi ameapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza uliokuwa huru nchini humo.

Alimshinda rais aliyekuwa mamlakani Moncef Marzouk.

Ushindi wake unaaminisha kwamba Tunisia ndilo taifa ambalo limejinasua kutoka utawala wa kiimla hadi ule wa kidemokrasia.

Siku ya jumatatu,tume ya uchaguzi ilithibitisha kuwa bwana Essebsi alishinda kura ya raundi ya pili dhidi ya Marzouk.

Rais huyo ameapishwa katika bunge la wawakilishi wapwa ambapo chama chake Nidaa Tounes kina wabunge wengi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia wa Tunisia wakisherehekea ushindi wa Caid Essebsi

.Hatua hiyo hiyo inafikisha tamati mvutano wa demokrasia wa miaka minne ya ghasia zilizoghubika taifa hilo zilizopeleekea kung'olewa kwa utawala wa Rais Zine el-Abedine Ben Ali.

Bwana Essebsi alihudumu katika utawala wa Ben Ali, pamoja na uongozi wa rais wa zamani Habib Bourguiba.