Watu 20 wafariki harusini Afghanistan

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mmoja ya watoto waliojeruhiwa wakati bomu liliporushwa katika nyumba moja iliokuwa ikifanya sherehe ya harusi mkoani Helmand nchini Afghanistan.Takriban watu 20 waliaga dunia

Sherehe moja ya harusi nchini Afghanistan, imeshambuliwa kwa mzinga uliorushwa na roketi na kusababisha mauaji ya watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya kumi na mbili.

Kisa hicho kilitokea wakati wa makabiliano makali kati ya walinda usalama wa Afghanistan na wapiganaji wa Taliban katika jimbo la Helmand.

Mmiliki wa jumba lilofanyiwa harusi hiyo amesema kuwa wageni walikuwa wanajikusanya nje kumkaribisha bi harusi,na kuongezea kuwa watoto wake tisa wametoweka.

Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Lashkar Gah,mji mkuu wa mkoa huo.

Shambulio hilo limetokea wakati wa siku ya mwisho kwa ujumbe wa wanajeshi wa Marekani na wale wa shirika la kujihami la NATO wanaoondoka nchini Afghanistan.