Kano wapokea mwaka mpya mara ya kwanza

Image caption Mwaka mpya 2015 ulivyopokelewa Hong Kong

Mwaka mpya wa 2015 umepokewa kwa kishindo katika maeneo mbali mbali duniani na barani Afrika.

Nchini Nigeria kumekuwa shamra shamra ambapo kwa mara ya kwanza mafataki yalirushwa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo lenye waislamu wengi.

Shamra shamra hizo zimefanyika katika kituo cha michezo katika mji wa Kano ambapo waliohudhuria ni wale waliopata mwaliko pekee.

Habari zinasema kumekuwa na mwitikio mkubwa ambapo umati wa watu ulihudhuria shamra shamra hizo jambo lililowapa wakati mgumu maafisa usalama kuudhibiti umati huo.

Waandaji wa shamra shamra hizo za maonyesho ya kulipua mafataki hayo wanasema wanataka jimbo la Kano kuungana na miji mingine mikubwa duniani kusherehekea siku kuu ya Mwaka Mpya.

Ulinzi mkali uliimarishwa kwa tahadhari ya shambulio lolote kutoka kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram.