Papa: Mwaka mpya akemea ufisadi Roma

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Papa Francis

Papa Francis ametumia sherehe za kuupokea mwaka wa 2015 kuzungumzia tatizo la rushwa katika mji wa nyumbani wa Rome nchini Italia.

Akizungumza katika Kanisa kuu la St. Peter Basilica, papa amesema rushwa ni shumbulizi dhidi ya maskini na wasiokuwa na uwezo ambapo ametaka mabadiliko ya kiroho na kimaadili katika mji huo.

Papa ambaye ndiye Askofu wa Rome amefanya utetezi dhidi ya maskini kama nguzo muhimu katika uongozi wake wa upapa.

Maafisa wa polisi kwa sasa wanawachunguza maafisa wa Roma wanaotuhumiwa kujihusisha na kundi la Mafia na ufisadi dhidi ya fedha za umma zikiwemo zilizotengwa kwa ajili ya kituo wahamiaji.