Polisi wapigwa kalamu kwa ubakaji India

Haki miliki ya picha Reuters File Photo
Image caption Maafisa wawili wa polisi nchini India wamepigwa kalamu baada ya kupatikana na hatai ya ubakaji

Waziri mkuu wa jimbo kubwa zaidi nchini India la Uttar Pradesh amewafuta kazi polisi wawili wanaoshtumiwa kwa kumteka nyara na kum'baka msichana wa umri wa miaka 14 siku ya Jumatano.

Akhilesh Yadav aliamrisha hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya polisi hao .

Mahakama ilisema kuwa polisi walimlazimisha msichana huyo kuingia ndani ya gari lao alipotoka nyumbani kwenda msalani .

Kisha walimpeleka kwenye kituo cha polisi ambapo walim'baka .