Jeshi la DRC kuwakabili waasi wa FDLR

Image caption Wanajeshi wa DRC

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inasema kuwa iko tayari kundesha oparesheni ya kijeshi dhidi ya waasi wa kihutu mashariki mwa nchi hiyo.

Waasi hao walishindwa kutii matakwa yaliyowekwa na jamii ya kimataifa miezi sita iliyopita ya kuwataka kuweka chini silaha na kuondoka eneo hilo lililo kwenye mpaka na Rwanda.

Waasi hao wa kihutu wanaojulikana kama FDLR wamekuwa wakitumia eneo la mashariki mwa Congo kama ngome yao ya kuipiga vita serikali ya Rwanda huku wakikisiwa kuhusika kwenye mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994

Ni karibu waasi 300 tu waliojisalimisha kati ya waasi wanaokisiwa kuwa takriban 1500.