Mwanasiasa ashtakiwa kwa kulangua watoto

Image caption Aliyekuwa Spika Hama Amadou

Mwanasiasa mashuhuri na maafisa kadha kutoka jeshini pamoja na wafanyibiashara wamefikishwa mahakamani nchini Niger kwa mashtaka ya kuhusika kwenye ulanguzi wa watoto.

Aliyekuwa spika wa bunge Hama Amadou anakabiliwa na mashtaka licha ya kutokuwepo mahakamani.

Alikimbilia ufaransa mwezi Agosti kufuatia kuibuka kwa madai hayo akisema kuwa yalichochewa kisiasa.

Watu 17 walikamatwa mwezi juni kwa kushukiwa kuhusika kwenye ulanguzi wa watoto kati ya Niger, Benin na Nigeria.

Kesi Hiyo imeahirishwa hadi mwisho wa mwezi huu.