Mitandao yakataa ubaguzi wa kidini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtu anayetumia mtandao wa facebook kwa mawasiliano

Mitandao ya Twitter na facebook imekataa kuchapisha mamia ya jumbe za chuki licha ya kutakiwa kuchapisha jumbe hizo na makundi ya ubaguzi .

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na gazeti la The Independent nchini Uingereza, idadi ya jumbe baadhi yao zikiwa zinawashtumu waislamu kwa kuwa wabakaji na kuwafananisha na ugonjwa wa saratani zimeongezeka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miezi iliopita baada ya kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia katika eneo la Rotherham na mauji ya mateka wa Uingereza yaliofanywa na kundi la Isis.

Facebook imesema kuwa iliamua kuzingatia usawa kati ya uhuru wa kujieleza na kuimarisha mazingira yalio salama,lakini pia ikasema kuwa haitakubali kuchapisha jumbe zinazowaingilia watu wengine kutokana na rangi au dini.

Twitter kwa upande wake imesema kuwa inazipitia jumbe zote zinazokiuka sheria zake zinakataa matamshi yoyote yanayoweza kuzua vurugu.