Majeshi ya DRC yapambana na waasi

Haki miliki ya picha
Image caption Wanajeshi wa DRC, katika mapambano

Vikosi vya Jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya kongo vinaudhibiti mji wa Abya ulioko kaskazini mashariki mwa mji wa Beni .

Vikosi hivyo, maarufu FARDC, vinaushikilia mji huo katika shambulio walilolifanya mwishoni mwa wiki, ambalo liliungwa mkono pia kikosi vya umoja wa mataifa ya kulinda usalama MONUSCO.

Ushindi huo wa jeshi la Congo umekuja baada ya mapigano makali na waasi wa Uganda ADF.

Katika shambulio hilo lililodumu zaidi ya saa sita, waasi watano waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa.