Israel:Wanajeshi wetu hawaendi ICC

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa hatakubali wanajeshi wake kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC.

Alikuwa akizungumza katika kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri tangu Palestina ilipotuma ombi la kujiunga na mahakama ya ICC ambayo wana imani itaifungulia mashtaka Israel kwa madai ya uhalifu wa kivita katika maeneo inayokalia.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Israel imesema kuwa wanajeshi wake hawatakwenda mbele ya mahakama ya IIC kujibu mashtaka

Bwana Netanyahu ameishtumu Palestina kwa kutumia njia ya mapambano.

Israel imezuia kitita cha dola millioni 125 ufadhili wa fedha za kila mwezi kwa Palestina kama kodi inayochukua kwa niaba yake kama makubaliano ya mkataba wa amani.

Hatahivyo Palestina imepinga hatua hiyo ikitaja kama adhabu dhidi yake.