Mlipuko mkubwa wasikika Mogadishu

Image caption Mlipuko Mogadishu

Ripoti kutoka Somali zinasema kuwa mlipuko mkubwa umesikika karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Mogadishu.

Haijulikani ni nini kilichosababisha mlipuko huo lakini walioshuhudia wanasema kuwa wameripoti kusikia milio mikali ya risasi baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka katika makutano ya barabara moja katikati ya mji huo.

Moshi mweusi ulionekana ukifuka katika eneo hilo.

Usalama umeimarishwa mjini Mogadishu katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni,lakini kundi la wapiganaji la Al Shabaab limekuwa likitekeleza mashambulizi.