Jenerali Ssejusa arudi Uganda

Haki miliki ya picha AFP
Image caption rais wa Uganda, Yoweri Museveni

Rais wa Uganda amekutana kwa mara ya kwanza na Jenerali David Ssejusa aliyekuwa uhamishoni nchini Uingereza.

Aidha amesema suala la kurudi nyumbani kwa jenerali huyo kutoka uhamishoni alilishughulikia yeye mwenyewe bila ya kushirikisha mtu yeyote.

Rais Yoweri Museveni pia ameamuru polisi wa jeshi la UPDF waliokuwa wamezunguka nyumba ya Jeneri huyo na kumzuia kwa muda wa siku kadhaa bila kutoka nje waondoke nyumbani kwake.

Wanasheria wa Jenerali Ssejusa wamefahamisha pia ombi la kutaka kustaafu jenerali huyo limekuwa likijadiliwa.

Jenerali huyo wa Uganda alikaa uhamishoni nchini Uingereza zaidi ya mwaka mmoja na nusu baada ya kukashifu sera za Rais Museveni, kumuachia madaraka mwanaye mara baada ya kustaafu kwake.