Vijana wakamatwa kwa uhalifu, Tanzania

Image caption Polisi wa Tanzania wakilinda doria

Jeshi la polisi nchini Tanzania linawashikilia baadhi ya vijana wanaotuhumiwa kufanya vurugu kwa kuwapora watu mali.

Kundi la kihuni la vijana linalojulikana kama ''Panya Road'' lilifanya vurugu kwa kuwapora watu mali zao na kwenye maduka ya mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.

Msemaji wa jeshi la Polisi nchini humo Advera Bulimba amesema vijana 36 walikamatwa na wanahojiwa.

Amefahamisha kuwa vijana hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi ukikamilika.

Aidha Msemaji wa jeshi la Polisi amefafanua kuwa ''Panya Road'' ni vikundi vidogo vidogo vya watoto wahuni wanaojiingiza katika vitendo vya uhalifu.