Urusi kuruhusu askari kutoka nje

Image caption Meli za ulinzi za Urusi

Urusi imeanza kuruhusu askari kutoka nje wenye utalaam ili kuingia katika jeshi lake.

Hata hivyo, wataalam wa Urusi wanasema hatua hiyo haina uhusiano wowote na mgogoro nchini Ukraine.

Rais Vladimir Putin ameidhinisha sheria inayowawezesha raia wa kigeni kufanyakazi angalau kwa miaka mitano katika jeshi la Urusi ili mradi wanajua kuzungumza Kirusi.

Wataalam hao wanatarajiwa zaidi watatoka katika jamhuri za Asia ambazo awali zilikuwa sehemu ya muungano wa nchi za Soviet.

Wageni wa kujitolea, wakiwemo Warusi wamekuwa wakipigana nchini Ukraine. Hata hivyo Urusi imekuwa ikikana kupeleka majeshi yake huko.

Serikali ya Ukraine na nchi za magharibi wanasema Urusi imetuma silaha nzito na askari wenye utaalam wa hali ya juu kuwasaidia watu wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine.