Watetezi wa chama tawala Burundi wauawa

Image caption Siasa za chama cha CNDD

Polisi nchini Burundi wanasema kuwa wanaharakati kutoka kwa chama tawala CNDD-FDD wameuawa kwa kupigwa risasi katika mji ulio mashariki mwa nchi wa Gisuru karibu na mpaka na Tanzania.

Wanasema kuwa wanaume watano waliokuwa wamevaa sare za jeshi waliingia kenye eneo moja la burudani siku ya jumapli ambapo waliwafunga wanaharakati hao kabla ya kuwaua.

Kisha walienda kwenye ofisi za chama hicho ambapo walichoma bendera ya chama.

Msemaji wa chama hicho anasema kuwa wale waliohusika ni kutoka kwa kundi lenye siasa kali kutoka upinzani wenye mipango ya kuvuruga uchaguzi ambao utafanyika baadaye mwaka huu.