Ahukumiwa kwa utekaji na mauaji

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hussam Qawasmeh

Mwanamume mmoja mwenye asili ya Palestina,amekutwa na hatia ya kuandaa utekaji nyara na hatimaye mauaji ya vijana watatu wenye asili ya Israel huko West Bank,amehukumiwa na mahakama ya kijeshi ya Israel kifungo cha miaka mitatu .

Hussam Qawasmeh pia aliamuriwa kulipa faini ya dola za marekani elfu sitini na tatu kama fidia kwa kila familia iliyokumbwa na mpango wake.

Watu wengine wawili waliokuwa wakishukiwa kutekeleza mpango huo,mapema mwezi June ,wao walipigwa risasi na kufa na jeshi la Israel mnamo mwezi Septemba mwaka jana Kitendo hicho cha utekaji nyara hatimaye mauaji ya vijana hao yalisababisha kuibuka kwa vurugu kubwa kati ya Israel na Palestina.