Mbwa atelekezwa na mkoba wake Uingereza

Haki miliki ya picha SPCA
Image caption Watetezi wa wanyama wameonywa watu kutowafuga wanyama makwao wakati hawawezi kuwatunza

Shirika moja la kutetea wanyama nchini Uingereza linamtafuta mmiliki wa Mbwa aliyepatikana akiwa ametelekezwa katika kituo cha treni nchini Scotland.

Inaarifiwa Mbwa huyo alipatikana akiwa ametelekezwa na vitu vyake ndani ya mkoba uliokuwa kando yake.

Jibwa hilo dume aina ya (Shar-Pei), lilipatikana wiki jana likiwa limefungwa kwa mnyororo katika chuma kimoja ndani ya kituo hicho.

Kando yake ulikuwa mkoba ambao ndani yake kulikuwa na mto wa kulalia wa mbwa huyo, kifaa chake cha kuchezea, bakuli alilokuwa anatumia kwa chakula pamoja na chakula chake.

Shirika hilo la kutetea maslahi ya wanyama, limewaonya wamiliki wa wanyama kutowatelekeza wanyama wao likisema ni hatia na pia kuwasahi watu kutowanunua wanyama kama vile Mbwa kwa sababu ya kutaka kuonekana tu kuwa na Mbwa nyumbani kwao.