Pakistani kuunda mahakama za kijeshi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistani, Chaudhry Nisar

Bunge nchini Pakistani limepitisha maamuzi ya kuundwa kwa mahakama za kijeshi kwa ajili ya kuwashtaki Wanamgambo wanaoshutumiwa kutekeleza vitendo vya kigaidi.

Mabadiliko haya ya Katiba ya Pakistani ni sehemu ya mfululizo wa hatua zinazochukuliwa kupambana na wimbi la mashambulizi yanayotekelezwa na wanamgambo wa Taliban ikiwemo mauaji dhidi ya watoto wa shule mwezi uliopita.

Vyama vingi vimebariki hatua hiyo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa mahakama za kiraia zimeonyesha kushindwa kuwafikisha wanamgambo kwenye mikono ya kisheria.

Waziri wa mambo ya ndani,Chaudhry Nisar Ali Khan amesema mahakama za kijeshi zitakuwa na mamlaka kwa kiasi fulani.