Mkia wa ndege Air Asia wapatikana

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkia wa Ndege wa Air Asia umepatikana bahari ya Java

Mkia wa ndege ya Air Asia iliyoanguka umepatikana kwenye bahari ya Java, kikosi cha kilichokuwa kikisaka ndege hiyo kimeeleza.

Mkia huo wa ndege hutunza visanduku vyeusi vinavyorekodi mawasiliano ndani ya ndege ambavyo vingeweza kuwasaidia wachunguzi kubaini chanzo cha ajali.

Sehemu hiyo ya mabaki ya ndege ilionekana kwenye eneo la ziada lililoongezwa kwenye operesheni ya kutafuta ndege hiyo.

Air Asia ilipotea ilipokuwa ikitoka Surabaya, Indonesia kwenda Singapore tarehe 28 mwezi Desemba ikiwa na Watu 162.

Hakuna manusura yeyote aliyepatikana.

Mpaka sasa miili 40 pekee imepatikana lakini Mamlaka zinaamini kuwa abiria wengi zaidi wamenasa ndani ya ndege hiyo.