Al-Shabaab ladai kuwaua majasusi wa USA

Image caption Wapiganaji wa kundi la Alshabaab wamedai kuwaua wapelelezi wanne wa Marekani nchini Somali

Wapiganaji wa kundi la Alshabaab kutoka Somalia wanasema kuwa wamewaua watu wanne wanaodaiwa kuwa wapelelezi wa Marekani,Ethiopia na serikali ya Somalia.

Wanne hao wanadaiwa kupigwa risasi katika mji wa Baradhere siku ya jumanne baada ya jaji mmoja wa Alshabaab kuwapata na hatia ya kuwaunga mkono wapelelezi wa CIA na mashirika yanayokabiliana na kundi hilo.

Wiki iliopita maafisa wa Somali wanasema kuwa shambulizi moja la ndege lililotekelezwa na Marekani lilimuua kiongozi wa ujasusi wa Alshabaab Abdishakur Tahlil.