Steven Gerrard akaribishwa LA

Image caption Kobe Brayan

Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Kobe Brayant katika kuonyesha umoja michezoni amemtumia ujumbe nahodha wa timu ya Liverpool Steven Gerrard, baada ya uthibitisho kutoka timu ya LA Galaxy kwamba kiungo huyo mkabaji ataungana na timu hiyo mwaka huu.

Katika ujumbe wake wa video kwa Steven, Brayant anamwambia mchezaji huyo wa zamani wa timu ya England kuwa yeye ni shabiki wake wa muda mrefu na kwa hilo Brayant anaamini ushindi mwingine unakuja kwa timu ya Galaxy, na anathibitisha ushindi upo, maana ana imani na Steven Gerrard.

Gerrard atakipiga katika ligi kubwa za vilabu baada ya mkataba wake wa awali na Anfield kumalizika.