Ethiopia:Watimuliwa kutoka ardhi yao

Image caption Jamii ya wafugaji inalazimika kubadili utamaduni wao

Kujengwa kwa bwawa kubwa nchini Ethiopia na kuanza kwa kilimo cha biashara ilikua kazi kubwa kubaini Watu wa jamii hiyo wanafikiria nini, lakini kwa msaada wa chupa ya pombe ya kienyeji hakuna lililoshindikana.

Baada ya kusubiri kwa wiki kadhaa barua ya ruhusa kutoka kwa mamlaka mbalimbali za wizara nchini Ethiopia, ninaanza safari yangu kuelekea kusini mwa nchi hiyo.

Katika eneo hilo kuna jamii ya wafugaji ya watu takriban 100,000,ambao baadae walibadilika kuwa wakulima wa bidhaa za kibiashara.

Katika Bonde la Omo wana historia waligundua baadhi ya mabaki ya binadamu wa kwanza.

Wakati nikisonga mbele zaidi katika bonde hilo nawasili katika kijiji kimoja nina matumaini ya kuzungumza na jamii iitwayo Mursi, kundi la Watu takriban 7000 maarufu kwa kuvaa vyuma kwenye midomo yao.

Image caption Bwawa la Gibe III

Utamaduni wa maisha yao hivi sasa uko hatihati ya kuisha, hivi sasa wametulia wakijihusisha na kilimo katika ardhi yao hivyo kuondokana na utamaduni wao wa awali wa kutembea huku na huko kuchunga ng'ombe.

Nilipopata nafasi ya kuuliza kwa mmoja wa Wazee wa jamii hiyo alisema ''Serikali inatuambia tuuze Ng'ombe wetu na tubadilike kama watu wa mjini'' wanasema ardhi yetu ni mali ya mashirika ya Sukari, hatujaulizwa tunataka nini.

''ikiwa hatutakubaliana nao tutapelekwa Jela, je tutaishije ikiwa hatuwezi kuwa na ardhi, Ng'ombe wala maji?