Aliyepandikiza mbegu kwa mkewe awa Baba

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gerardo Hernandez akiwa na mkewe Adriana Hernandez

Jasusi wa nchini Cuba aliyeachiliwa na Marekani hivi karibuni hivi sasa amekuwa Baba baada ya ombi lake la kutaka mbegu zake za kiume zikapandikizwe kwa mkewe wakati alipokuwa jela.

Mbegu za Gerardo Hernandez zilisafirishwa kwenda Cuba alikokuwa mkewe.Hernandez alikua akitumikia kifungo nchini Marekani kwa makosa ya kufanya vitendo vya kijasusi, lakini aliachiwa mwaka jana yakiwa ni matunda ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba.

Cuba na Marekani zilitangaza mwezi Desemba kuwa nchi hizo zimerejesha uhusiano wa kidiplomasia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1961.