Misri yadumisha ulinzi mpakani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeshi la Misri

Jeshi nchini misri linaripotiwa kuanza kutekeleza mpango wa kupanua eneo lake lenye ulinzi mkali kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na ukanda wa Gaza.

Zaidi ya nyumba 1000 zitabomolewa karibu na eneo lililo karibui na mpaka huo.

Hii ndiyo oparesheni ya pili ya ubomoaji wa nyumba za wakazi na itaongeza mara dufu ukubwa wa eneo hilo la ulinzi.

Jeshi la misri linapambana na wanamgambo kaskani mwa Sinai na lina mipango ya kuzuia usafirishaji wa silaha kupitia kwa njia za chini kwa chini kati ya Misri na ukanda wa Gaza.