Dhamana ya mshukiwa wa pembe yakataliwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pmbe za ndovu

Mahakama moja nchini Kenya imetupilia mbali ombi la kuachiliwa kwa dhamana Feisal Mohammed Ali anayeshukiwa kuwa mlanguzi mkubwa wa pembe za ndovu.

Mahakama hiyo ya Mombasa imesema Ali huenda akahepa mkono wa sheria, jinsi alivyotorokea Tanzania kesi yake ilipoanza.

Uamuzi wa Feisal Mohammed Ali kutorokea Tanzania wakati alipokuwa akitafutwa na Polisi sasa umemgharimu uhuru wake.

Mahakama ya Mombasa imesema mshukiwa huyo alikuwa anajua kesi yake imeanza alipoamua kusafiri hadi Tanzania mnamo Juni 2014.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption ndovu

Aidha mahakama imesema hatua hiyo na sababu tosha ya kukataa kumwachilia kwa dhamana.

Polisi walimkamata Feisal nchini Tanzania mnamo Disemba mwaka jana, na kumshitaki kwa kulangua kilo 314 za pembe za ndovu.

Kesi yake itaendelea tarehe 20 Januari.