Dawa ya nyoka ni nyoka

Nyoka aitwaye dragon snake Haki miliki ya picha Photoshot Holdings Ltd Alamy

Wanasayansi wa Uingereza wanasema kuwa wanatengeneza dawa kwa watu wanaotafunwa na nyoka wenye sumu kali, katika nchi za Afrika kusini ya Sahara.

Watafiti katika chuo kikuu cha matibabu ya magonjwa ya nchi za joto cha Liverpool, wanakusanya protini kutoka sumu za nyoka wakali kama 400 na wataongeza kemikali ili dawa iweze kuhimili joto.

Wananyonya sumu ya nyoka kama 80 kila wiki.

Inakisiwa kuwa watu 30,000 wanakufa kila mwaka kwa sababu ya kutafunwa na nyoka.