Somalia yaandaa mkutano wa IGAD

Haki miliki ya picha
Image caption mkutano wa OIgad wafanyika Somali kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miongo mitatu

Mawaziri wa mataifa ya Afrika mashariki wamekamilisha mkutano wao wa kihistoria katika mji mkuu wa Somali Mogadishu.

Ni mara ya kwanza katika kipindi cha mda wa miongo mitatu kwa shirika la IGAD kuandaa kikao chake nchini Somalia.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka nchini Somalia mnamo mwaka 1991 na migogoro imeendelea hadi sasa.

Mkutano huo ulifanyika katika hoteli iliokuwa na ulinzi mkali karibu na serikali ya mji mkuu wa Mogadishu.

Maafisa wa Somali wanasema kuwa maandalizi ya mkutano huo ni ishara ya udhabiti unaoimarika.

Hatahivyo mapigano kati ya serikali na kundi la Alshbaab yanaendelea nchini humo.