Papa Francis ziarani Sri Lanka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Papa Francis

Papa Francis amewasili nchini Sri Lanka ambako anatarajiwa kusisitiza umhimu wa mazungumzo baina ya makundi mbalimbali ya imani hasimu za kidini nchini humo.

Pia Papa Francis akiwa nchini humo aanatarajiwa kuhimiza ala la maridhiano wakazi walio wengi wa visiwa vya Sinhalese na wale wachache wa kisiwa cha Tamil.

Hii ni ziara ya kwanza kwa Papa Francis kutembelea taifa hilo tangu ziara ya kwanza ya Papa ya mwaka 2009.

Rais wa sasa wa Sri Lanka Maithripala Sirisena ameahidi kukomesha ubaguzi wa kidini visiwani humo.