Wabunge Burkina Faso kukatwa mishahara

Image caption Bunge la Burkina Faso

Wabunge wa bunge la Burkina Faso wamekubali kupunguza mishahara yao kwa asilimia hamsini.

Wameamua kufanya hivyo baada ya kutokea cheche za maneno kati ya wabunge hao kwenye mitandao ya kijamii baada ya taarifa kutolewa kwamba wabunge ambao huhuduria vikao katika bunge la Ouagadougou hupokea zaidi ya dola elfu tatu kama mishahara kila mwezi.

Mshahara wa kawaida wa wafnyakazi nchini humo ni karibu dola miamoja hamsini kila mwezi.

Kulingana na mbunge mmoja kutoka katika chama cha (Transition National Council (CNT), mshahara wao unajumuisha marupupu ya kuhudhuria vikao vya bunge , kulipia ofisi ,bima ya afya na ya kununua petroli.

Lakini kwa mujibu wa mwanaharakati mmoja Herve Kam wabunge hao hawapaswi kupokea marupurupu ya kuhuhduria vikao vya bunge.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa Rais Blaise Compaore aliong'olewa mamlakani mwezi Oktoba mwaka jana

Amesema ana wasiwasi kwamba mishahara ya wabunge iko juu sana ikilinagishwa na kipato cha wanachi wa kwaida wanaowpaigia kura kuwawakilisha bungeni.

Herve anasema kuwa mshahara wa kati ya dola 720 na 900 unawatosha wanasiasa hao ikilinagishwa na kiwango cha maisha nchini humo.

Rais Blaise Compaore aling'olewa mamlakani mwezi Oktoba mwaka jana.

Mmoja wa wabunge alinukuliwa akisema anapenda mshahara wanaopokea kwa sababu itawafanya wabunge kutetea demokrasia na kurejesha imani wa watu katika demokrasia.

Mishhara hio imewakera wengi kwenye mitandao ya kijamii nchini Burkina Faso wakiilaani na kusema haionyeshi usawa huku wakitoa wito wa wabunge kupunguza mishhara yao.