Waliouawa Ufaransa kuzikwa leo

Image caption Majeneza ya baadhi ya waliouawa nchini Ufaransa ambao watazikwa mjini Jerusalem

Mazishi ya wachora vibonzo saba wa jarida la Charlie Hbdo waliouawa wiki jana yanafanyika leo mjini Paris.

Watu wangine wanne waliouawa katika duka kubwa watazikwa mjini Jerusalem.

Katika hafla nyengine ya mazishi ya polisi waliouawa katika mashambulizi hayo wanapewa maziko ya heshima ambayo imehudhuriwa na Rais Francois Hollande.

Wiki jana Ufaransa iligubikwa na mshtuko na taharuki kwa siku tatu wakati ndugu wawili waliposhambulia jarida la Charlie Hebdo kutokana na hasira kwamba jarida hilo lilimkejeli mtume Muhammad wa dini ya kiisilamu.

Kwa jumla watu 17 waliuawa na vijana hao wakiwemo wandishi wa habari.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waathiriwa wanne wa mauaji katika duka la wayahudi mjini Paris

Katika makao makuu ya polisi mjini Paris, Bwana Hollande aliwatwika polisi watatu wlaiouawa katika mashambulizi hayo mataji ya heshma kwa kazi yao ya kulinda nchi na hasa kwa kupoteza maisha yao wakifanya hivyo.

Mjini Jerusalem mazishi yanafanyika ya watu wengine wanne ,Yoav Hattab, Philippe Braham, Yohan Cohen na Francois-Michel Saada -waliouawa ndani ya duka lililomilikiwa na wayahudi. Watazikwa katika kakaburi ya Har HaMenuhot.

Miili yao iliwasili mjini humo asubuhi ya leo.

Taharuki ilitanda Ufaransa kwa siku tatu baada ya vijana wawili ambao walikuwa ndugu Said na Cherif Kouachi kushambulia ofisi za jarida hilo la Charlie Hebdo. Wlaioshuhudia mashambulizi hayo wanasema vijana hao walisikika wakisema kwa sauti kwamba wamemlipizia kisasi Mtume Muhammad , baada ya kuwaua wandishi hao.

Baadaye vijana hao waliuawa na polisi.