Hatutawabagua Waislam:Ujerumani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kansela Angela Merkel na viongozi wengine wakitoa salam za rambi rambi shambulizi la Ufaransa

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck amewahakikishia uvumilivu na ustahimilivu waislam million nne waliopo nchini humo pamoja na tukio la shambulizi nchini Ufaransa.

Katika kumbukumbu ya shambulio la mjini Paris Ufaransa mbele ya umati, Rais Gauck alisema “sisi wote ni Wajerumani”. Amesema kuwa walitekeleza shambulio Charlie Hebdo nia yao ni kutaka kuwagawa watu kwa matabaka ya dini,lakini Ujerumani kamwe haiwezi kufuuata mgawanyiko huko kwa Waislam waliopo Ujerumani. Awali viongozi wa kidini na kisiasa pamoja na Kansela Angela Merkel walitoa salam zao za rambi rambi kwa kuweka maua ubalozi wa Ufaransa nchini Ujerumani kama hatua ya kulaani shambulio hilo.