Gazeti lenye kibonzo cha Mtume lauzwa

Haki miliki ya picha AFP

Gazeti la Charlie Hebdo leo limeanza kusambaza toleo la gazeti lake ambalo limechapishwa kibonzo cha Mtume Mohammad kwenye ukurasa wake wa mbele.

Nakala Milioni za gazeti hilo zimeanza kusambazwa na nyingine zitafuata iwapo wanunuzi wataongezeka.

Picha ya kibonzo hicho iliyopo ukurasa mbele wa gazeti hilo inamwonyesha Mtume Mohammad akilia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wandishi wa jarida la Charlie Hebdo wamechapisha tena picha ya kibonzo cha mtume Muhammad

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa picha hiyo itachochea chuki.

Hata hivyo waandishi wa habari wa gazeti hilo wanasema ukurasa wa mbele unamaanisha Waandishi wa habari wamewasamehe waliotekeleza shambulizi la kigaidi lilolofanyika jumatano wiki iliyopita.

Naibu Mhariri wa Gazeti la Liberalation Alexandra Schwatzbrod anasema ulikuwa uamuzi mwepesi kwa gazeti lake kuchapisha picha ya kibonzo hicho..