Colombia:Serikali,FARC kupata muafaka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Silaha zilizokusanywa kutoka kwa wapiganaji wa FARC

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos anasema kuwa mazungumzo yenye lengo la kumaliza mapigano kati ya Serikali na wanamgambo wa FARC yataanza hivi karibuni.

Mazungumzo hayo yanaelezwa kumaliza mzozo wa muda mrefu na wapiganaji hao wa mrengo wa kushoto.

Katika ujumbe wa mwaka mpya uliotolewa siku ya jumatano, Santos amesema mchakato wa amani uko katika awamu za mwisho, ambapo Rais huyo amesema ni muhimu sana kwa mustakabali wa vizazi vya sasa na vijavyo.

Maswala yanayotiliwa mkazo ni pamoja na maswala ya haki za waathiriwa na kumaliza mzozo nchini Colombia.

Rais Santos amesema wameanza mchakato wa makubaliano juu ya namna watakavyowezesha wapiganaji kuacha silaha na kuingia katika maisha ya uraia.