Jarida lakaidi na kuchapisha kibonzo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tayari vitosho vimetolewa dhidi ya wamili wa jarida hilo la Uturuki

Jarida la Cumhuriyet nchini Uturuki, ndilo pekee katika mataifa ya kiisilamu lililochapisha picha ya kibonzo cha kumkejeli mtume Muhammad iliyokuwa kwenye toleo la Jumatano la jarida la Charlie Hebdo.

Hatua hii inasemekana ilikuwa ni ishara ya umoja na kuwauna mkono wachora vibonzo waliouawa nchini Urafansa wiki jana.

Bila shaka jarida hilo la Uturuki ndilo pekee katika nchi za kiisilamu lilichapisha picha za kibonzo hicho. Kilikuwa kibonzo cha picha ya mtu anayedaiwa kuwa mtume Mohammad akilia baada ya kukasirishwa na yaliyowakumba wachoraji vibonzo wa Charlie Heblo.

Wandishi wawili wa jarida hilo walitumia picha hiyo ndani ya gazeti hilo la Uturuki, ingawa picha hio haikuchapishwa kwenye ukurasa wa kwanza wa jarida lenyewe.

Nakala mpya ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo lilitolewa baada ya wachora vibonzo wake 8 kuuawa na vijana waisilamu na llichapishwa katika lugha sita ikiwemo kiarabu na kiturki.

Tayari vitisho vimetolewa dhidi ya wamiliki wa jarida hilo baada ya uamuzi wake wa kuchora kibonzo kingine kumkejeli mtume Mohammad

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Suiku moja baada ya mashambulizi ya Ufaransa, kichwa cha habari cha jarida la Cumhuriyet kilisema '' wameua mawazo mapya''

Jarida hilo katika lugha ya kiarabu lilichapishwa tu kwenye mtandao,lakini nchini Uturuki kibonzo hicho kilichapishwa na jarida la Cumhuriyet, ambalo linaunga mkono upinzani na kuifanya Uturuki kuwa nchi pekee ya kiisilamu duniani kuchapisha kibonzo hicho.

Jarida hilo la Cumhuriyet lilichapisha vibonzo vingine kwenye kurasa nne kama hatua yao ya kuwaunga mkono wachoraji wa Ufaransa.

Siku moja baada ya mashambulizi nchini Ufaransa dhidi ya jarida la Charlie Heblo, kichwa cha habari cha jarida la Cumhuriyet kilisema: ''waliua mawazo mapya''

Lakini waandishi wawili wa jarida hilo Ceyda Karan na Hikmet Çetinkaya, waliamua kutumia kibonzo hicho katika taarifa zao katika kurasa za ndani ya gazeti hilo, ingawa picha walizotumia zilikuwa ndogo ikilinganishwa na ile iliyokuwa katika jarida la Charlie Heblo.

Jarida hilo linasema kuwa ofisi zao zilivamiwa na polisi lakini baadaye wakaruhisiwa kuuza nakala za magazeti yao baada ya polisi kuhakikisha kwamba hawakuwa na picha hio.

Cumhuriyet linasema kuwa tayari limepokea vitisho na kwamba ofisi zao ziko chini ya ulinzi wa polisi.

Wandishi hao wawili waliotumia kibonzo hicho wanasema kwamba serikali ya sasa inakandamiza sana uhuru wa watu kujieleza na kwamba watu wanapaswa kuruhusiwa kuwepo na imani nyinginezo sio moja tu.