Republican yampinga Obama

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Barack Obama na Spika wa bunge John Boehner

Wabunge wa chama cha Republican ambao ni wengi Marekani wanapinga mipango ya Rais Barack Obama kuzifanyia mabadiliko sera za Uhamiaji nchini humo.

Spika wa bunge la Marekani John Boehner amesema hatua ya serikali iliyotangazwa na Rais Obama mwezi Novemba mwaka jana haikuwa imeidhinishwa na bunge la taifa hilo.

Lakini Ikulu ya Marekani imesema chama cha Republican kimechukua hatua ambazo si sahihi kupinga hatua ya Rais Obama akuhusiana na marekebisho ya sera ya uhamiaji ili kuwapa uraia wasioa raia wa taifa hilo.