Bei ya mafuta yafuta ajira, Schlumberge

Image caption Mtambo wa kuchimba Mafuta

Kampuni kubwa ya uzalishaji wa mafuta Duniani ya Schlumberger imesema itapunguza ajira kwa kiwango cha asilimia saba kutokana na kuanguka kwa bei ya mafuta ulimwenguni.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahudumu wa vituo vya Mafuta wakosa kazi

Hatua hiyo ya kupunguza wafanyakazi inakuja kufuatia hali iliyotarajiwa ikiwemo matarajio kidogo ya tofauti na gharama ya ugunduzi na uzalishaji wa mafuta kwa mwaka 2015. Makampuni tanzu ya mafuta ya Schlumberger yamepunguza ghrama za uchimbaji mafuta kutokana na anguko hilo la bei. Bei ya mafuta katika soko la Dunia imeanguka kwa zaidi ya asilimia 50 tangu mwezi June mwakajana hali inayoathiri mataifa ambayo yamekuwa yakinufaika na biashara za mafuta Duniani.