Boko Haram ishughulikiwe kimataifa

Rais John Mahama wa Ghana Haki miliki ya picha AFP

Rais wa Ghana, John Mahama, ameiambia BBC kwamba msaada wa kimataifa unahitajika kuweza kulishinda kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, nchini Nigeria.

Rais Mahama alisema nchi moja pekee haiwezi kuwashinda wapiganaji hao na kwamba ugaidi kila pahala ni tishio la dunia nzima.

Rais wa Ghana alisema viongozi wa nchi za Afrika Magharibi watakutana juma lijalo kuomba idhini ya Umoja wa Afrika kuunda kikosi cha kimataifa ili kupambana na Boko Haram, lakini aliongeza kusema kuwa kutuma kikosi hicho kunaweza kuchukua miezi.

Wanajeshi wa Chad wameanza kujongea Cameroon, kama sehemu ya ushirikiano zaidi wa kanda hiyo dhidi ya Boko Haram.