Dominic Ongwen wa LRA akabidhiwa kwa ICC

Dominic Ongwen (kulia) akipeana mkono na kamanda wa kikosi cha AU kutoka Uganda huko CAR Haki miliki ya picha bbc

Kiongozi muandamizi wa kundi la wapiganaji wa Uganda, Lord's Resistance Army, ambaye anashutumiwa kutenda uhalifu dhidi ya binaadamu, apelekwa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, mjini Hague Jumamosi.

Dominic Ongwen aliwekwa kizuizini na wanajeshi wa Marekani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kusallim amri siku 10 zilizopita.

Ijumaa, afisa wa mashtaka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alisema Dominic Ongwen, ambaye aliajiriwa na LRA tangu akiwa mtoto, amekabidhiwa kwa wawakilishi wa ICC.

Kundi la LRA linaloongozwa na Joseph Kony limewateka maelfu ya watoto ili kupigana na kuwaowa.