Mafuriko yawaua watu 170 Malawi

Image caption Mafuriko Malawi

Takriban watu 170 wanaripotiwa kuaga dunia kwenye mafuriko ambayo yameikumba Malawi kwa karibu mwezi mmoja sasa.

Watu wengine 100,000 wamelazimika kuhama makwao.

Mapema wiki hii rais Peter Mutharika alitangaza thuluthi moja ya nchi hiyo kuwa katika hali ya hatari na kuomba msaada wa kimataifa.

Zaidi ya watu wengine 50,000 wamehama makwao katika nchi jirani ya Msumbuji kutokana na mafuriko hayo.