USA kuamua kuhusu ndoa za jinsia moja

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mahakama ya Marekani kufanya uamuzi wa jumla kuhusu ndoa za jinsia moja nchini humo

Mahakama kuu nchini Marekani inatarajiwa kutoa uamuzi wa nchi nzima iwapo wapenzi wa jinsia moja wana haki ya kufunga ndoa.

Mahakama hiyo itatathmini suala hilo kwenye majimbo ya Kentucky, Ohio, Michigan, na Tennessee kati ya majimbo mengine 14 ambayo yamepiga marufuku ndoa za jinsia moja.

Mahakama hiyo pia itaamua ikiwa majimbo yatatambua ndoa za jinsia moja kutoka sehemu nyengine nchini humo.

Kukubaliwa kwa ndoa za jinsia moja kumeshuhudiwa nchini Marekani miaka ya hivi karibuni suala ambalo linaungwa mkono pakubwa na chama cha Democratic huku likikigawanya chama cha Republican.