Wanne wafariki kutokana na bomu Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bomu lawaua watu wanne Nigeria

Ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu wanne na kuwajeruhi wengine kadhaa katika shambulizi la kituo cha basi huko Potiskum.

Mji huo umekuwa ukishambuliwa na wapiganaji wa boko haram kwa mara kadhaa sasa.

Jumapili iliopita walipuaji wawili wa kujitolea muhanga walijilipua na kuwaua watu wanne katika soko moja lililojaa watu.

Wachanganuzi wanakadiria kwamba hadi watu elfu 13 wamefariki tangu kundi la boko haram lianzishe harakati zake mnamo mwaka 2009.