Mamilioni wahudhuria misa ya papa Manila

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Papa francis

Kiongozi wa kanisa katoliki papa francis anaongoza misa ambayo imehudhuriwa na watu wengi katika bustani ya Rizak kwenye mji mkuu wa Ufilipino Manila akiwa kwenye siku ya mwisho ya ziara yake barani Asia.

Waandalizi wanasema kuwa watu milioni kadhaa wamehudhuria misa hiyo licha ya kuwepo kwa mvua.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Papa Francis

Misa hiyo inatajwa kuwa iliyohudhuriwa na watu wengi zaidi tangu papa John Paul wa pili azuru eno hilo mwaka 1995.

Picha za televisheni zilionyesha watu wengi katika bustani ya Razal wakipunga mikono na kushangilia wakati papa alipokuwa akipita akiwa ndani ya gari lake.