West Ham yapanda katika ligi ya EPL

Haki miliki ya picha Getty
Image caption West Ham yatamba

West Ham wamerudi katika nafasi nzuri ya kushiriki katika mechi za kilabu bingwa Ulaya baada ya kuicharaza mabao matatu bila jibu Hull City.

Hull City ilidhibiti mchezo katika kipindi cha kwanza lakini mabao ya Andy Carroll na Morgan Amalfitano yalitosha kuinyamazisha Hull City katika uwanja wa nyumbani.

Ushindi huo unaiweka West Ham sawa na Arsenal katika jedwali la ligi ya Uingereza kabla ya Arsenal kupambana na Mancity.

Hull City nayo inakabiliwa na tishio la kushushwa katika ligi hiyo.